
Joseph Hezron (54), fundi seremala, Mkazi wa Bukara, wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, akituhumiwa kuchoma nyumba ya mpenzi wake, Lucy James (51), mkulima na mkazi wa Ibisabageni, akimtuhumu kuwa ana mahusiano na mwanaume mwingine aliyejulikana kwa jina la Jeremia Kamambi (53), na kusababisha hasara ya mali zilizokuwa kwenye nyumba hiyo zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Mil. 16/=, kisha kujaribu kujiua kwa kujijeruhi na kitu chenye ncha kali shingoni.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imebainisha kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 09, 2023 majira ya 1:00 Jioni ambapo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifanikiwa kuuzima moto huo kabla haujaleta madhara makubwa, pia lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo aliyekuwa amejificha porini, baada ya kutenda uhalifu huo, na kwamba anaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Sengerema.

