Back to top

Watanzania wameshauriwa kuchangia damu kuokoa maisha ya wajawazito.

23 March 2018
Share

Watanzania wamehizwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara, lengo likiwa kuokoa maisha ya mama wajawazito wakati wa kujifungua, watoto wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na wagonjwa wengine wenye mahitaji ya damu.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Khairaati Islamic mara baada ya kujitolewa kuchangia damu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi Sokoine.