
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, amewasili Jijini The Hague, Uholanzi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 13 - 15 Novemba 2023.



Pamoja na mambo mengine, Mhe. Makamba ataongoza ujumbe wa Tanzania katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji Kati ya Tanzania na Uholanzi litakalofanyika tarehe 14 na 15 Jijini The Hague.
Aidha, pembezoni mwa kongamano hilo, Mhe. Waziri Makamba atapata nafasi ya kukutana na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Uholanzi, Mhe. Kanke Bruins Slot. Kadhalika, Mhe. Makamba anatarajiwa pia kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi (Tanzania Diaspora).
Aidha ujumbe wa Waziri Makamba umehusisha wafanyabiashara 16 kutoka sekta binafsi za Tanzania ambao watashiriki kwenye kongamano hilo.
