
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo, amewataka wawekezaji wa Biashara ya Cabon nchini, kuwa wawazi katika biashara hiyo.
Ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi ya malipo ya shilingi bilioni 47 kwa wakazi wa Wilaya za Kiteto na Mbulu, ambazo zimenufaika na mradi huo mkoani Manyara leo Novemba 14, 2023.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Jafo amewaelekeza wawekezaji kuwa na vyeti vinavyoonesha mahali walipouza bidhaa zao, ili kuwa wawazi kwa mujibu wa kanuni ya 4 ya Sheria ya Mazingira inayowataka kuwa na uwazi katika biashara zao.
