Back to top

RAIS SAMIA AELEKEZA WANANCHI KULIPWA FIDIA BILA USUMBUFU

16 November 2023
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza wananchi wote wanaopisha miradi ya maendeleo kulipwa fidia zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.

Silaa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa ulipaji fidia za wananchi katika kupisha Mradi wa Uchimbaji wa Madini ya Nickel, unaofanywa na Kampuni ya Tembo Nickel katika Halmashauri ya Manispaa ya Ngara mkoani Kagera.

Katika ziara hiyo ambayo imehudhuriwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Silaaameitaka Kampuni Tembo Nickel kulipa fidia za wananchi kwa haraka kabla ya tarehe 25 Disemba 2023.