
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dakta. GANCHWELE MAKENGE amesema, maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI mkoani humo yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Dakta MAKENGE amewahimiza wananchi kuendelea kupima afya zao ili kujua kama wameambukizwa au la.
Ametoa kauli hiyo Mjini Lindi kwenye uzinduzi wa kampeni wa ya upimimaji wa saratani za matiti na mlango wa kizazi, kifua kikuu na magonjwa yasio ya kuambukiza.