Back to top

ISRAEL, HAMAS KUSITISHA VITA KWA SIKU 4

22 November 2023
Share

Israel na kundi la Hamas, wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku 4, makubaliano ambayo yatashuhudia kundi hilo likiwaachia mateka 50 iliyowachukua tangu Octoba 7, pande hizo mbili zimethibitisha.

Baraza la mawaziri la Israel limeidhinisha makubaliano hayo yanatarajiwa kuanza Alhamisi asubuhi ambapo angalau mateka 50 wanawake na watoto wanatarajiwa kuachiwa 

Na makubaliano hayo pia yalionyesha kuwa siku ya ziada itaongezwa kwa kila mateka 10 wa ziada watakaoachiliwa.

Wafungwa 150 wa Kipalestina wataachiliwa kutoka jela za Israel kama sehemu ya makubaliano, Hamas ilisema katika taarifa yake. 

Israel pia imetoa orodha ya wafungwa 300 wa Kipalestina ambao hatimaye wanaweza kuwa sehemu ya makubaliano mapana ya kuwaachilia mateka wanaoshikiliwa huko Gaza.