Back to top

SUA kuanzisha chuo kutatua migogoro ya wanyama pori na wananchi

23 March 2018
Share

Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinie - SUA - Mkoani Morogoro kinatarajia kuanzisha Kituo cha Mafunzo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma ambacho tafiti zake zinatarajiwa kuondoa migogoro mingi iliyopo kati ya wanyamapori wakimwemo tembo na wananchi.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo kutakapojengwa kituo hicho eneo la Muhuwesi, Mkuu wa Idara ya Wanyamapori katitka Chuo Kikuu cha Sokoine, Profesa NSAJIGWA EMMANUEL amesema  kituo hicho kitatumika na wanafunzi kwa elimu ya vitendo kikiwa maalum kwa mafunzo ya wanyamapori.

Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa wilaya ambazo zimekuwa na migogoro mingi inayotokea kati ya wananchi na wanyamapori wakiwemo tembo ambapo wananchi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kushambuliwa na wanyamapori na mazao ya mashamba yao kuharibiwa hivyo tafiti za chuo hicho zitasaidia kuondoa migogoro hiyo.