
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa amesema amegundua migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na watu anao waita viongozi na vinara wa uvamizi wa maeneo nchini.
Waziri Silaa ameyasema hayo mkoani Iringa, wakati akipokea taarifa ya Utekelezaji wa Baraza la Mawaziri kuhusu Vijiji 975 vilivyo na migogoro ya mipaka ya hifadhi, mipaka ya misitu na vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali nchini.


Silaa amesema katika kipindi chake cha Waziri wa Ardhi amegundua viongozi wengi wamekuwa vinara wa uvamizi wa maeneo na ardhi za watu wengi, jambo ambalo limekuwa likisumbua kila siku.
Amesema, kwa muda mrefu kumekuwa na viongozi ambao ni vinara wa uvamizi wanaotumia vyombo mbalimbali vya sheria na maafisa wakubwa wa Serikali katika kuvamia na kudhurumu maeneo ya watu.
