Back to top

WAWILI WAKUTWA NA TUHUMA KIFO CHA MARIAM

27 November 2023
Share

Watumishi wawili wamekutwa na tuhuma za kujibu kufuatia kifo cha Bi. Mariam Zahoro mkazi wa Kijiji cha Mumbwi kilichopo wilayani Handeni, mkoani Tanga, kilichotokea kwenye Kituo cha Afya Kabuku.
.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu,  baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi wa kifo cha mama Huyo pamoja na kichanga chake katika kituo hicho cha Afya.
.
Akifafanua Taarifa hiyo Waziri Ummy amesema, Kamati imebaini kuwa Daktari wa zamu namba 2 alishindwa kufika kwa wakati kutoa huduma za dharura licha ya kupewa taarifa mara kwa mara ya kutakiwa kufika Kituoni kutoa huduma ya dharura kwa mgonjwa huyo.
.
Amesema, Daktari huyo licha ya kufika Kituoni kwa kuchelewa bado alishindwa kutimiza wajibu wake wa kitaaluma ikiwemo kutoa rufaa kwa mgonjwa kwenda kuhudumiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni (ambayo ipo takribani kilometa kutoka Kituo cha Afya Kabuku) baada ya mtaalamu wa usingizi kutopatikana kwenye simu na hivyo mgonjwa kutofanyiwa upasuaji kwa wakati. 
.
Aidha Kamati imebaini ukiukwaji wa Maadili kwa Muuguzi mwenye utaalamu wa kutoa huduma ya dawa ya usingizi ambapo imepelekea kutakiwa kutoa maelezo ndani ya siku 14.