
Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, limewataka waandishi wa habari kujali usalama wao, pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kutafuta habari na kuuhabarisha Umma, pamoja na kujua mipaka ya kazi yao, pindi wanapotimiza majukumu yao.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya, wakati wa mdahalo wa awamu ya pili ya majadiliano kati ya Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe, na Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC).
“Waandishi wa habari ni vyema kuzingatia usalama wako kwanza wakati unatekeleza majukumu yako ya kukusanya taarifa sehemu zenye vurugu au sehemu nyingine ni bora kujiangalia wewe kwanza na sio kuhatarisha maisha yako katika mazingira hatarishi ambayo yanaweza kukusababishia madhara ambayo unaweza kuyaepuka”.Kamanda Mallya.
