
Serikali mkoani Tanga imetaifisha bidhaa mbali mbali ikiwemo mifuko ya sukari zaidi ya 300, ndoo za mafuta ya kula zaidi ya 200 pamoja na majahazi mawili vyote vinavyokadiria kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 kwa kuingiza bidhaa hizo bila kulipia ushuru.
Akizungumza baada ya kukagua bidhaa hizo zilizokamatwa katika mwambao wa bahari ya Hindi vikisafirishwa kuingia jijini Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bwana MARTIN SHIGELLA amesema serikali itaanza operesheni ya kuhakiki baadhi ya viongozi wa serikali wanaoshirikiana na wafanyabishara wanaoingiza bidhaa zao nchini bila kulipia ushuru kisha kuwakamata wafanayabiashara husika.
Kwa upande wake, Meneja Msaidizi -Forodha na Ushuru bidhaa Bwana EDWAERD NDUPA amesema bidhaa hizo zingeikosesha serikali zaidi ya shilingi milioni 15.
Kufuatia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga amabaye aliongoza opereshenia ya kukamata bidhaa hizo EDWARD BUKOMBE amesema operesheni ya kukamata magendo ni endelevu.