
Hali ya huzuni imetanda katika eneo la Kapweria, katika kaunti ya Narok baada ya msichana wa miaka 13 kumuua mamake kwa kutumia Panga wakati mama akipambana kumnyang'anya simu binti yake.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Transmara Mashariki Boniface Kavoo, anasema mtuhumiwa huyo, aliokota panga na kumvamia mama yake mwenye umri wa miaka 55 na kumkata kichwani.
Bw Kavoo alisema majirani waliosikia vilio kutoka kwenye makazi ya mtuhumiwa walienda na kukuta mama wa binti huyo akigaagaa kwa maumivu na kuomba msaada huku akiwa anavuja damu nyingi.
“Ni mazingira ambayo mama yake alitaka kumpokonya simu binti yake aliyokuwa anatumia, inaonekana marehemu hakufurahishwa na msichana wake kufanya mawasiliano mengi bila yeye kujua. njia zote za kumpigania mama yake, jambo ambalo liliishia katika umauti,” aliongeza afisa huyo.
Binti huyo inasemekana alitupa silaha ya mauaji kwenye shimo la choo ili kuficha ushahidi lakini baadaye alikiri kumuua mamake kwa kile alichodai hakumpa uhuru.
