Back to top

KINARA WIZI WA MIFUGO ADAKWA KAGERA

16 December 2023
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, linamshikilia Jasson Rwegasira maarufu kwa jina la Mbelwa, akituhumiwa kuwa kinara wa genge la waharifu wanaojihusisha na wizi wa mifugo katika maeneo mbalimbali mkoani humo na mikoa jirani ya Simiyu na Geita.
.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi, mkoani humo, ACP Balsius Chatanda, amesema Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa wilayani Nzega mkoani Tabora, baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu, ambapo aliwahi kukimbilia mkoani Dar es Salaam ambako alifanikiwa kuwakimbia Polisi, akaenda nchini Burundi ambako nako aligundua kuwa anafuatiliwa ndipo aliporudi Nzega.