
Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), wamefanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye mabasi ya abiria na kubaini baadhi ya wamiliki na mawakala wa mabasi kuwapandishia nauli wananchi huku mamlaka hiyo ikiwapiga faini kwa kosa la kuzidisha nauli hizo.
Akiongea katika ukaguzi wa nauli hizo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Arusha SSP Zauda Mohamed amesema wapo katika ukaguzi wa nauli kutokana na malalamiko ya wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii kuhusiana na kupanda kwa nauli.
Ameongeza kuwa kwa sasa ukataji tiketi ni kwa mfumo wa kielektroniki ambapo amesema kuna mifumo mipya inayorahisisha kuangalia bei elekezi ya serikali huku akiwaomba abiria kutumia mifumo hiyo ili kutokuumizwa na nauli kandamizi.
