
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Mabunge Duniani (IPU), Dr.Tulia Ackson, wametajwa katika orodha ya wanawake 100 wenye ushawishi zaidi Afrika kwa mwaka 2023.
.
Orodha hiyo imetolewa na mtandao wa Avance Media, ambapo baadhi vigezo vilivyotumika ni pamoja na ubora katika uongozi na utendaji, mafanikio binafsi pamoja na Kujitolea katika mambo mbalimbali.

