
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imempa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Bwana ABDUL NONDO.
Mahakama hiyo imetoa dhamana kwa masharti ya wadhamini wawili ku tia saini dhamana ya Shilingi Milioni 5.
Mahakama hiyo imesema kumnyima dhamana mtuhumiwa huyo ni kumnykima haki yake ya kusoma, hivyo apewe dhamana ili siku ya kesi ahudhurie kesi na siku nyingine aendelee na masomo.
Kesi ya Bwana NONDO itatajwa tena tarehe 10 mwezi ujao.