
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewataka mawakala wa mabasi, kuandika taarifa kikamilifu ili kuwapa haki abiria kipindi inapotokea swala la malipo ama ajali.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha, na Bw. Johansen Kahatano, Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka LATRA, wakati wakifanya ukaguzi wa mabasi katika Kituo kikuu cha mabasi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani.
Mkurungenzi huyo amewataka Mawakala wa mabasi, kuandika taarifa kamili za abiria ambazo zipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za LATRA, Pia kuandika vyema utambulisho wa mizigo ya abiria ili kuondoa changamoto ya upotevu wa mizigo ya abiria.
