
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango, ametoa wito kwa Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na waumini mara baada ya kushiriki Ibada ya Mwaka Mpya katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma.
Amesema ni muhimu Watanzania kuendelea kukemea na kupinga utengano, udini, ukabila pamoja na siasa za chuki, halikadhalika Makamu wa Rais amewasihi watanzania kufanya kazi kwa bidii, maarifa na nidhamu ili kuinua maisha ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.
