Back to top

RAIS RUTO ADAI MAHAKAMA INATUMIKA KUMUHUJUMU

04 January 2024
Share

Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kuishutumu idara ya Mahakama ya nchi hiyo, kwa kile anachokitaja kuwa inatumika kuhujumu miradi yake na kudai kuwa baadhi ya majaji wamepewa hongo ili kutoa maamuzi mabovu dhidi ya utawala wake.
.
Kufuatia kauli hiyo Viongozi mbalimbali wa upinzani, Mawakili na Idara ya Mahakama, wameukashfu usemi huo, wakisema kuwa haufai nani wa kiimla, huku Jaji Mkuu wa Mahakama nchini humo, Martha Koome, akiwataka Majaji na wafanyakazi wa Mahakama kutotishwa na yeyote wanapotekeleza majukumu yao.
.
Hata hivyo kupitia mtandao wa X zamani Twitter, Rais Ruto amesema kuwa atafanya kila juhudi kupambana na ufisadi katika Idara ya Mahakama, licha ya baadhi ya Viongozi wa upinzani, wakiwemo wabunge kumtuhumu kula njama ya kuiteka idara hiyo, kama ambavyo wamedai kuwa tayari ameliteka Bunge la nchi hiyo na kwamba Bunge hilo ni kibaraka wa Rais huyo.