Back to top

INDIA YAFIKISHA CHOMBO CHAKE KWENYE ORBIT YA JUA

07 January 2024
Share

Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa India, Jitendra Singh, amesema nchi hiyo imefanikiwa kufikisha chombo chake cha anga za mbali kwenye mzingo (orbit) wa jua, baada ya safari ya miezi minne ya chombo hicho, yenye lengo la kuifanyia utafiti nyota hiyo iliyozungukwa na sayari mbalimbali ikiwemo dunia.
.
Akitoa taarifa hiyo Singh amesema mafanikio hayo yamemfurahisha Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi, ambaye amesema kuwa hatua hiyo ni "alama ya kihistoria" kwa India katika miradi yake ya anga za mbali.
.
Chombo hicho kilichopewa jina la Aditya-L1, kilirushwa mnamo mwezi Septemba 2023 kikiwa kimebeba vyombo vya kisasa vya kupima na kuchunguza tabaka la juu la Jua, ambapo kimesafiri taribani kilometa milioni 1.5 kutoka uso wa dunia umbali ambao ni asilimia moja pekee kutoka duniani hadi lilipo jua. #via #dw