Back to top

ISOSO SECONDARY, FORM ONE WARIPOTI 6 KATI 138

11 January 2024
Share

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, amefanya msako katika mnada wa Mhunze, uliopo wilayani humo na kufanikiwa kukusanya wanafunzi zaidi ya 45 waliokuwa wanazurura mnadani wakati masomo yakiendelea.
.
Mkuu huyo wa Wilaya amefikia uamuzi huo baada ya kukagua mahudhurio ya wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Isoso iliyopo wilayani humo na kukuta wanafunzi wa kidato cha kwanza watatu tu kati ya 138 waliotakiwa kuripoti kwenye shule hiyo.
.
Akizungumza na ITV Mkuu wa Shule ya Sekondari Isoso, Bi.Anusiata Audax, amesema wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa kwenye shule hiyo ni 138 ambapo wasichana ni 85 na wavulana 53, lakini hadi leo Januari 11, 2024, walioripoti ni wanafunzi 6, wavulana wakiwa 5 na msichana mmoja.