
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango, amewataka wazazi na walezi nchini kuacha tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu majumbani na kuwakosesha haki ya kupata elimu.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Skuli ya Msingi ya Elimu Mjumuisho Jendele iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja,ikiwa ni shamrashamra zaMaadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema ni vema watoto hao wakapata elimu ili kuweza kutumia vipaji walivyonavyo kwani serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia ikiwemo ya shule jumuishi.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amalim Zanzibar, Mhe.Lela Muhammed Mussa, amesema kukamilika kwa mradi huo ni jitihada zinazofanywa na serikali, ili kuhakikisha elimu inapatikana katika mazingira mazuri.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kufanya mapinduzi makubwa ya kielimu ambapo yanajumuisha uboreshaji wa miundombinu, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuongeza vifaa vya kisasa katika vituo vya kutolea elimu.
