Back to top

PINDA ATIA MGUU MIGOGORO YA ARDHI UWANDANI DODOMA

12 January 2024
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda ameingia uwandani kutatua na kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake ya migogoro ya ardhi katika Jiji la Dodoma.

Mhe. Pinda Katika kutafuta suluhu ya eneo hilo, ameagiza mmiliki wa eneo analodai, Kisiju kumiliki afike ofisini kwake na nyaraka zote za umiliki kwa lengo la kupata muafaka wa mgogoro huo.

Pinda aliambatana na watendaji wa sekta ya ardhi Makao Makuu ya Wizara, Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma na wale wa Jiji la Dodoma ambapo alitembelea eneo la Chang’ombe, mbapo Bi.Dorothy alibomolewa kimakosa ukuta wa nyumba yake na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambapo ameelekeza mwananchi huyo kujengewa ukuta.

"Ninyi mnaoishi hapa sura ya ujirani lazima itengenezwe kwa kuepuka migogoro ya ardhi katika maeneo yenu, mnataka mpaka waziri aje ndiyo atengeneze ujirani"Amesema Pinda

Aidha, alitembelea eneo la Chang’ombe Extension, ambapo mwananchi mmoja, Ramadhani Kisiju anadai kumiliki kiwanja alichokuwa akilima kwa muda mrefu.

Uamuzi wa Pinda kutembelea na kukagua maeneo ya mgogoro uwandani unafuatia kuwasilishwa kwa malalamiko ya migogoro ya ardhi kwake, huku baadhi ya malalamiko yakihusisha watendaji wa sekta ya ardhi.