
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imetangaza kusitisha kibali cha Shirika la Ndege la Kenya (KQ) cha kuendesha safari za ndege za abiria kati ya Nairobi na Dar es salaam.
.
Maamuzi hayo yamefuata baada ya Mamlaka ya Anga ya Jamhuri ya Kenya kukataa ombi la Tanzania, kwa Kenya kusafirisha mizigo yake yote kwa kutumia Kampuni ya Air Tanzania, kwa kuzingatia makubaliano ya Huduma za Anga kati ya Tanzania na Kenya yaliyotiwa saini mnamo Novemba 24, 2016, Jijini Nairobi nchini Kenya.
.
Hivyo kufuatia uamuzi huo hakutakuwa na safari za ndege za abiria za ndege za Shirika la ndege la Kenya KQ kati ya Nairobi na Dar Es Salaam kuanzia January 22, 2024.
