Back to top

WATAHINIWA 1,330, LESENI YA UKUNGA WAFUTIWA MATOKEO

16 January 2024
Share

Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania, limetangaza kufuta matokeo ya mtihani wa usajili na leseni za wauguzi na wakunga kwa watahiniwa wa Stashahada 1,330, uliofanyika Septemba 07, 2023.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, imebainisha kuwa Baraza Hilo limefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa kuna kuvuja kwa mitihani hiyo katika ngazi ya Stashahada na kwamba mtuhumiwa aliyehusika na uvujaji huo, tayari amebainika na amesimamishwa kazi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
.
Kufuatia hatua hiyo, Baraza hilo limesema watahiniwa watapewa nafasi ya kufanya mtihani mwingine bila malipo yoyote, ambao utafanyika Februari 16, 2024, mkoani Dodoma.