
Rais wa Liberia anayemaliza muda wake George Weah, amesema hana mpango wa kutaka kuchaguliwa tena mwaka 2029 baada ya kushindwa katika uchaguzi wa hivi majuzi.
Bw.Weah, mwanasoka wa zamani wa kimataifa, alichaguliwa mwaka wa 2017 lakini akashindwa katika uchaguzi wa Novemba na Joseph Boakai, ambaye anatazamiwa kuapishwa Jumatatu.
Bw.Weah amesema alihitaji "wakati kwa ajili yangu, watoto na familia".
Katika hotuba yake iliyosifiwa na watu wengi mwezi Novemba, Bw.Weah alisema chama chake cha Congress for Democratic Change (CDC) kitasalia kuwa upinzani mkali.
