Back to top

AC ROMA WAMFUNGASHIA VIRAGO MOURINHO

16 January 2024
Share

Klabu ya AS Roma, imetangaza kuachana na kocha wake, Jose Mourinho, kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo.
.
Roma wanaachana na Mourinho wakiwa wameshinda mchezo mmoja tu kati ya sita iliyopita kwenye Ligi ya Kuu ya Italia ‘Seria A’, ambapo katika mechi yao ya mwisho dhidi ya AC Milan waliambulia kichapo cha mabao 3-1, huku wakishika nafasi ya 9 kwenye ligi hiyo.
.
Imetajwa kuwa Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Daniele De Rossi, ndiye anapewa nafasi kubwa kumrithi Mourinho.