
Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limesema kuwa Kituo chake cha kufua umeme cha New Pangani, kimepata hitilafu kwenye mitambo yake, hivyo kusababisha kituo hicho kushindwa kuzalisha jumla ya megawati 68, na kupelekea upungufu kwenye gridi ya Taifa.
.
Shirika hilo limesema mikoa iliyoathirika na hitilafu hiyo ni Tanga, Kilimanjaro na Arusha na kwamba tayari wataalamu wake wanaendelea na matengenezo yanayotarajiwa kukamilika baada ya siku tano.

