
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, iliyopo mkoani Tanga, Bw.Isaya Mugishangwe Mbenje, kuanzia leo Januari 21, 2024, ili kupisha uchunguzi.
.
Hatua hiyo imefuata baada ya Mhe.Mchengerwa kupokea taarifa za Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kusababisha kulega lega kwa utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwenye Halmashauri hiyo.

