
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, ameagiza ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam kufunga kamera zenye sauti ili kufuatilia utoaji wa huduma kwa wananchi, baada ya kuwepo kwa malalamiko ya kutoridhishwa na huduma hiyo.
Waziri Silaa ameelekeza watumishi wote kuvaa vitambulisho pindi watoapo huduma, ili kusaidia utambuzi wa haraka wa mtumishi husika iwapo kutakuwa na malalamiko kuhusu utowaji wa huduma mbovu hasa lugha isiyofaa yanapobainishwa.
Waziri Silaa ameyasema hayo wakati alipotembelea Kituo cha Huduma kwa Mteja kilichopo Jijini Dar es Salaam, ili kujionea hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi hao.





Katika hatua nyingine waziri Silaa amewataka watumishi wote kufanya kazi kwa kujituma bila ya shinikizo kutoka mamlaka ya juu ya kiutendaji.
