Back to top

NDEGE YA JESHI LA URUSI YAANGUKA YAUA 74 WAKIWEMO WAFUNGWA WA UKRAINE

24 January 2024
Share

Ndege ya kijeshi ya Urusi iliyokuwa imebeba watu 74, wakiwemo wafungwa wa kivita 65 wa Ukraine, imeanguka katika Jimbo la Belgorod nchini Urusi na kusababisha vifo vya watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo, huku tukio hilo likidaiwa kuwa limefanywa ili kuhujumu zoezi la kubadilishana wafungwa.
.
Kufuatia kuanguka kwa ndege hiyo, aina ya Ilyushin II-76 iliyotengenezwa kwa ajili ya kubeba wanajeshi, mizigo na vifaa vya kijeshi, Wizara ya Ulinzi nchi hiyo imevituhumu vikosi vya Ukraine kuwa vimeidungua ndege hiyo kwa kutumia makombora waliyopewa na nchi za magharibi, ambapo imekitaja kitendo hicho kuwa ni cha kigaidi na kishenzi.
.
Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, wataalamu wa rada wa nchi hiyo wamegundua kuwa makombora mawili ya Ukraine yalirushwa kutoka kwenye Jimbo la Kharkiv, eneo linalopakana na Belgorod, wakati ndege hiyo ilipodunguliwa, hata hivyo, wizara hiyo haijatoa ushahidi wowote kuhusu madai hayo.