Back to top

MOROGORO: WANAFUNZI ZAIDI YA 40 WAPIGWA RADI

25 January 2024
Share

Wanafunzi zaidi ya 40 wa shule ya Sekondari Kingalu, iliyopo Kata ya Kilakala, Manispaa ya Morogoro, wamenusurika kifo baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa.
.
Akizungumza juu ya tukio hilo Mkuu wa Shule hiyo, Mwl.Miyango Msilanga, amesema radi hiyo ilipiga kwenye madarasa ya kidato cha kwanza na cha tatu, na kusababisha madhara kwa wanafunzi zaidi ya 40 ambapo baadhi yao walipoteza fahamu, huku 25 wakilazimika kupelekwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Morogoro kwa matibabu zaidi.
.
Hata hivyo, Mwalimu Msiyanga amesema wanafunzi 17 kati ya 25 ndiyo wamebaki hospitali wakiendelea na matibabu.