
Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, imetakiwa kushughulikia mara moja maeneo korofi kwenye barabara za ndani ya hifadhi hiyo ili watalii waweze kutembelea maeneo mengi wanapofika kwenye Hifadhi hiyo.
.
Agizo hilo limetolewa na Kamishna wa Hifadhi za Taifa nchini, Juma Kuji, alipotembelea hifadhi hiyo, ambapo amebainisha kuwa licha ya changamoto ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hawawezi kusubiri ziishe, lazima washughulikie maeneo yote korofi, huku lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha barabara zote kwenye hifadhi hiyo, zinapitika wakati wote.
.
Aidha, Kamishna huyo amesema miundombinu yote katika Hifadhi za Taifa nchini inaboreshwa ili kukidhi matamanio ya wageni wanaotembelea hizo.
