Back to top

MAAFISA WA MAHAKAMA WATAKIWA KUWA WAZALENDO.

28 January 2024
Share

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, mkoani Songwe, Bw. Solomoni Itunda, amewataka maafisa wa mahakama wakiwemo mawakili wa kujitegemea wanaopata nafasi ya kuwawakilisha Mahakamani wateja wao wakiwemo wanaotuhumiwa kwa kesi za  unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti kuwa wazalendo kwa kuacha kuwatetea wahalifu na badala yake  kuwasaidia waathirika pamoja na Mahakama hali ambayo itasaidia kupunguza vitendo hivyo.

Bw. Itunda ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, katika mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria inayoendelea nchini wakati akizungumza na wananchi pamoja na maafisa kutoka idara mbalimbali ikiwemo idara ya mahakama

Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa songwe bwana hassan makube licha ya kuwataka maafisa hao kusimamia haki amesema maadhimisho hayo yamelenga kutoa elimu kwa wananchi kwenye masuala ya kisheria.