
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 29.12.2023.
Akitangaza matokeo hayo katika Ofisi za Baraza Jijini Dodoma, Msajili wa Baraza Bi.Agnes Mtawa, amesema, Mtihani huo uliofanyika katika vituo nane vya mitihani hapa nchini, ulikuwa na jumla ya watahiniwa 4142 kwa ngazi za Stashahada, Shahada, na, Astashahada ya Uuguzi na Ukunga.
Bi.Mtawa amebainisha kuwa, Jumla ya Watahiniwa 2099 kati ya 4142 Wamefaulu mtihani huo, ambapo watahiniwa wa Ngazi ya SHAHADA waliofanya Mtihani ni 482 na waliofaulu Mtihani ni 346, Ngazi ya STASHAHADA waliofanya Mtihani ni 3608 na waliofaulu Mtihani ni 1737, na Ngazi ya ASTASHAHADA waliofanya Mtihani ni 52 na waliofaulu Mtihani ni 16, ambapo hali ya Ufaulu kwa ujumla imeongezeka kwa asilimia 4.7 ikilinganishwa na Mtihani uliofanyika Mwezi Disemba, 2023, ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 4.6 ya watahiniwa 4253.
Aidha, Bi.Mtawa ameongeza kuwa, Mitihani hii huendeshwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga Tanzania ya Mwaka 2010, kifungu cha 6 (o) Baraza linajukumu lakuandaa, kuendesha na kusimamia Mitihani ya Usajili au Uorodheshwaji, na Mitihani hii hufanywa mara tatu kwa mwaka, Mwezi Disemba, Machi na Agosti.
Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ni Mamlaka ya Kisheria iliyoanzishwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 na Kanuni zake, kwa lengo la kusimamia wanataluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga, ili kuhakikisha jamii inapata Huduma za Afya zilizo na Bora na Salama.
