
Serikali imewataka maafisa watendaji wa Vijiji na Kata kufanya utaratibu wa kiundendaji kwa kufuata taratibu za utumishi wa umma na kwa wale watakao kiuka hilo hatua za kiutumishi zitachukuliwa dhidi yao
Hatua hiyo ya serikali imejiri bungeni Jijini Dodoma wakati wa Kipindi cha Maswali na Majibu ambapo Mbunge wa Viti Maalu Mhe.Hawa Mwaifunga alipouliza swali la nyongeza akiuliza juu ya changamoto ya maeneo ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji watendaji kufanya shughuli zao kinyume na utaratibu huku akitaka kujua kuwa serikali ina mpango gani katika kutoa mafunzo kwa watendaji hao ili kufanya kazi kwa malengo waliyokusudiwa.
Swali hilo limejibiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Dkt.Festo Dugange amesema serikali itaendelea kuwajengea uwezo maafisa hao kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara.
