Back to top

Klabu ya AC Milan yapata kocha mpya.

09 October 2019
Share


Klabu ya AC Milan ya Italy imemteua kocha wa zamani wa Inter Milan Stefano Pioli kuwa kocha wao mpya baada ya kuachana na kocha wao Giampaolo kufuatia mwenendo mbovu wa timu hiyo kwenye ligi ya Italy Serie A.

Kocha Pioli alizaliwa Parma Oktoba 20 mwaka 1965, na alianza maisha yake ya ukocha mwaka 1999. Na mnamo mwaka 2006 alishiriki katika ligi ya Italy kwa mara yake ya kwanza kama kocha akiwa na timu ya Parma.

Kocha huyo anatajwa kuwa na uzoefu mkubwa kwani hadi sasa mbali na Parma amekwisha vifundiaha vilabu vingi nchini Italy kama vile Chievo Verona, Palermo, Bologna, Lazio and Inter, kabla ya kuifundisha Fiorentina tangu mwaka 2017.

Stefano Pioli amejiunga na AC Milan kwa makataba wa miaka miwili, na anatarajiwa kulipwa kiasi Euro mil 1.5 kwa mwaka huu.