Back to top

Kocha wa Lyon ya Ufaransa atimuliwa kazi.

08 October 2019
Share

Rasmi klabu ya soka ya Lyon ya Ufaransa imemtimua kazi kocha wake Sylvinho baada ya mwanzo mbaya kwenye ligi.

Sylvinho aliteuliwa kurithi mikoba ya kocha Bruno Genesio mwezi May lakini sasa kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 raia wa Brazili anatimuliwa baada ya timu hiyo kuanza vibaya ligi ya Ufaransa ikiwa timu hiyo imecheza michezo 9 tangu apewe majuku ya kuifundisha timu hiyo.

Lakini maamuzi hayo pia yamefuatia timu hiyo kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Saint-Etienne jumapili iliyopita.

Matokeo hayo yameifanya Lyon kushika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa ni nafasi ya inayoweza kuwafanya waingie katika idadi ya timu zitakazoshuka daraja licha ya kumaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita.