Back to top

Matumaini ya Chelsea kwa Wilian Borges Da Silva yarejea.

27 July 2020
Share

Klabu ya Chelsea ya Uingereza imefanikiwa kufanya mazungumzo tena na kiungo wao mshambuliaji Wilian Borges Da Silva na sasa wana matumaini ya kumuongezea mkataba mpya na kusalia ndani ya klabu hiyo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika msimu uliomalizika siku ya jana wa epl.

Wilian Borges Da Silva amekuwa akitaka kupewa mkataba wa miaka mitatu lakini Chelsea wao wakimpa ofa ya mkataba wa miaka miwili.

Lakini kwa mujibu wa ‘Sky sport’ ni kwamba licha ya ofa hiyo iliyotolewa na klabu ya Chelsea tayari wamefanikiwa kuafikiana juu ya mkataba mpya.