Back to top

Timu ya Espanyol ya Hispania yamfuta kazi kocha David Gallego.

08 October 2019
Share

Timu ya Espanyol ya Hispania imemtimua kazi kocha David Gallego wakati timu hiyo ikiwa katika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi kuu Laliga nchini na kumteua kocha wa zamani wa Sevilla Machin kuwa kocha wao mpya.

Klabu hiyo ilikuwa na kikao mapema jumatatu ya Leo na kufikia maamuzi hayo kumtimua kocha huyo kwani kocha huyo ameshinda mchezo mmoja tu msimu huu licha ya timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano ya Europa League.