Back to top

13 WAFARIKI KATIKA AJALI YA LORI NA HIACE, LINDI

22 April 2024
Share

Watu 13 wamefariki dunia huku 6 wakijeruhiwa baada ya Lori la mafuta kugongana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya HIACE, katika eneo la Somanga, wilayani Kilwa, mkoani Lindi.
.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameeleza kuwa majeruhi wote sita wamepelekwa katika hospitali ya Tingi, kwa ajili ya matibabu, na miili imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.