
Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu, amesema wagonjwa 13 kati ya 15 waliothibitika kuugua ugonjwa wa kipindupindu mkoani Dar es Salaam wamepona.
Ameeleza hayo mkoani Dar es Salaam , na kubainisha kuwa wagonjwa wengine wawili kati ya hao wanaendelea vizuri na wanaendelea kupatiwa matibabu.
