Back to top

7 WALIOFARIKI KWA KULA KASA, 3 MATATANI RUFIJI

14 March 2023
Share

Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji linawashikilia watuhumiwa watatu, kufuatia vifo vya watu saba kutoka kaya nne tofauti waliobainika kufariki dunia baada ya kula nyama ya samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, ACP Canute Msacky, amebainisha kuwa watuhumiwa hao watatu wanaoshikiliwa wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mafia baada ya kuzidiwa wakiwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi, kwani nao walikula nyama ya samaki huyo. 

Chanzo cha tukio hilo bado kinaendelea kuchunguzwa na Miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi wa Kitabibu katika hospitali ya Wilaya Mafia na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi. 

Pia Kamanda Msacky kwa ametoa onyo kwa wavuvi Wilaya ya Mafia kuacha tabia ya kuvua samaki aina ya kasa ambao ni nyara za Serikali, bali wafuate taratibu na sheria za uvuvi wa samaki hawa, Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kali kwa wavuvi wasiofuata taratibu na sheria za nchi. 

Waliofariki katika tukio hilo ni Abdalla Hatibu Nyikombo, 4yrs, Mshirazi na mkazi wa Bweni 2. Makame s/o Hatibu Nyikombo, 9yrs, Mwanafunzi S.t.d II S/Msingi Bweni 3. Mohamedi s/o Juma Makame, miezi 7, Mshirazi na mkazi wa Bweni 4. Ally s/o Selemani, miezi 8, mndengereko na mkazi wa Kanga 5. Salima d/o Omary Mjohi, 28yrs, Mshirazi, Mkulima na mkazi wa Bweni 6. Minza d/o Juma Hatibu, miezi 10, Mndengereko na mkazi wa Bweni na 7. Ramadhani s/o Karimu, miezi 8 Mndengereko na mkazi wa Bweni, aidha
marehemu hao walifariki majira tofauti tofauti.