
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ametaka tabia ya wakazi wa mkoa wa Manyara kuvamia mashamba ya watu wanaomiliki kwa hati ifike mwisho.
Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na watumishi wa sekta ya ardhi wa mkoa wa Manyara.
Kauli hiyo ya Waziri Silaa imekuja baada ya kubaini wamiliki wengi wa mashamba wanalalamika kuhusu kuvamiwa kwa mashamba yao na wananchi wenye Silaa za Jadi.