Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zimesababisha kifo cha mtu mmoja katika eneo la Stakishari Banana baada ya kuanguka ndani ya maji yaliyokuwa yamezingira nyumba za wakazi wa eneo hilo.
Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Augustino Mwenga amepoteza maisha baada ya kuanguka wakati akiwa katika harakati za kujilinda na athari za maji kujaa katika eneo hilo.