
Ajali iliyohusisha magari mawili ya kampuni ya Specialized Hauliers pamoja na kampuni ya saruji ya Dangote, yamegongana na kusababisha vifo vya madereva wa magari yote mawili, na majeruhi mmoja mkoani Lindi.
Ajali hiyo imehusisha gari namba T 393 DKA aina ya Howo mali ya kampuni ya Dangote, lililokuwa likiendeshwa na Daudi Mdota (40) iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea Mtwara, kugongana na gari namba T 234DZ T aina ya Howo mali ya kampuni ya Specialized Haulers LTD lilokuwa linaendeshwa na Jafari Omari.
Chanzo cha ajali kimetajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari namba T 393 DKA HOWO kutokuwa makini kwa watumiaji wengine wa barabara kwa kuhama upande wake wa kushoto na kuhamia kulia.
Miili ya marehemu imepelekwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Lindi, Sokoine kuhifadhiwa, pamoja na majeruhi aliyejulikana kwa jina la Saidi Mussa, ambae ameungua maeneo mbalimbali ya mwili wake nae akipelekwa hospitalini hapo kwa matibabu zaidi.