Back to top

BAA NA KUMBI ZA STAREHE 89 ZAFUNGIWA

08 May 2023
Share

Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limetangaza kuzifungia baa na kumbi za starehe 89, kutokana na maeneo hayo kusababisha kelele na mitetemo iliyozidi kiwango kinachotakiwa, ambapo miongoni mwa maeneo hayo ni Chako ni Chako, Kitambaa Cheupe, Element, Liquid, Rainbow Gentlemen, Soweto, Boardroom na Wavuvi Camp.
.
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa Baraza hilo, Samuel Gwamaka, amebainisha kuwa tayari walishawaonya na kuwaadhibu kwa kuwapiga faini lakini waliendelea kukaidi.