Back to top

Baadhi ya watumishi Ukerewe watuhumiwa kuhujumu fedha za mapato

14 February 2020
Share

Serikali mkoani Mwanza imebaini hujuma za wizi mkubwa wa fedha za mapato ya halmashauri ya wilaya Ukerewe kuibiwa wakati wa ukusanyaji kutoka kwenye vyanzo mbalimbali unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu katika maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara kutokana na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo kushindwa kuwasimamia

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amebainisha hali hiyo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake katika visiwa 29 vinavyokaliwa na wananchi wilayani Ukerewe kilichohudhuriwa pia na baadhi ya madiwani, wakuu wa idara,kamati ya ulinzi na usalama na watumishi wa halmashauri hiyo.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Ukerewe George Nyamaha ameahidi kushirikiana na wataalamu ili kumaliza tatizo  hilo na kuwataka watumishi kubadilika katika suala la ukusanyaji wa mapato. 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ameahidi kuanzisha mfumo wa kufanya ukaguzi kila wiki kwa kipindi cha miezi sita, huku akipiga marufuku kutoa fedha zitokanazo na mapato nje ya mfumo wa serikali.