
Mbunge Jimbo la Kinondoni, Abbas Tarimba, wakati akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Utamaduni na Michezo, Bungeni Jijini Dodoma, ameishauri serikali kuweka masharti kwa kampuni za michezo ya kubahatisha (Betting) kudhamini timu za Ligi Kuu ili kupata leseni ya biashara hiyo hapa nchini.
"Sports Betting inategemea sana mpira wa miguu, hapa Tanzania, 90% ya wanaocheza Betting, wanabet katika mpira wa miguu, hivyo industry ile inafaidika na mpira wa miguu, tunarudisha nini?...kwa hali hii nilikuwa nashauri serikali...iwe ni sharti la kikanuni kupata leseni kwa makampuni ya betting...ilazimike kudhamini Premier Club ama Championiship Club, hapo tutakwenda kusaidia nchi yetu katika michezo" Abbas Tarimba - Mbunge Jimbo la Kinondoni
